1
Wengi wamejitahidi kuweka katika mpangilio simulizi kuhusu masuala ambayo yametimizwa kati yetu,
2
kama walivyotupatia sisi, ambao tangu mwanzo ni mashahidi wa macho na watumishi wa ujumbe.
3
Hivyo nami pia, baada ya kuchuguza kwa uangalifu chanzo cha mambo haya yote tokea mwanzo - nimeona ni vema kwangu pia kukuandikia katika mpangilio wake - mheshimiwa sana Theofilo.
4
Ili kwamba uweze kujua ukweli wa mambo uliyofundishwa. Yesu
5
Katika siku za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani fulani aliyeitwa Zekaria, wa ukoo wa Abiya. Mke wake alitoka kwa binti za Haruni, na jina lake aliitwa Elizabeti.
6
Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu; walitembea bila lawama katika amri zote na maagizo ya Bwana.
7
Lakini hawakuwa na mtoto, kwasababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
8
Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.
9
Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.
10
Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.
11
Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.
12
Zakaria alitishika alipomuona; hofu ikamwangukia.
13
Lakini malaika akamwambia, "Usiogope Zakaria, kwasababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.
14
Utakuwa na furaha na uchangamfu, na wengi watafurahia kuzaliwa kwake.
15
Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
16
Na watu wengi wa Israel watageuzwa kwa Bwana Mungu wao.
17
Atakwenda mbele za uso wa Bwana katika roho na nguvu ya Eliya. Atafanya hivi ili kurejesha mioyo ya baba kwa watoto, ili kwamba wasiotii wataenenda katika hekima ya wenye haki. Atafanya hivi kuweka tayari kwa Bwana watu ambao wameandaliwa kwa ajili yake."
18
Zakaria akamwambia malaika, "Nitawezaje kujua hili? Kwasababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana."
19
Malaika akajibu na kumwambia, "Mimi ni Gabrieli, ambaye husimama mbele za Mungu. Nilitumwa kukwambia, kukuletea habari hii njema.
20
Na tazama, hutaongea, utakuwa kimya, hutaweza kuongea mpaka siku ile mambo haya yatakapotokea. Hii ni kwasababu ulishindwa kuamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati mwafaka."
21
Sasa watu walikuwa wakimsubiri Zakaria. Walishangazwa kwa kutumia muda mwingi hekaluni.
22
Lakini alipotoka nje, hakuweza kuongea nao. Wakatambua kwamba alikuwa amepata maono alipokuwa hekaluni. Aliendelea kuonesha ishara na alibaki kimya.
23
Ikatokea kwamba siku za huduma yake zilipokwisha aliondoka kurudi nyumbani kwake.
24
Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema,
25
"Hili ndilo amabalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu."
26
Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti,
27
kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.
28
Akaingia nyumbani kwake akasema, "Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe."
29
Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake.
30
Malaika akamwambia, "Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu.
31
Na tazama, utabeba mimba katika tumbo lako na utazaa mwana. Nawe utamwita jina lake 'Yesu.'
32
Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.
33
Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
34
Mariamu akamwambia malaika, hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote?
35
Malaika akajibu na akamwambia, "Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu.
36
Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.
37
Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu."
38
Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako." Kisha malaika akamwacha.
39
Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea.
40
Alikwenda nyumbani kwa Zakaria na akamsalimia Elizabeti.
41
Ikawa, Elizabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake tumboni, Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
42
Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, "umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
43
Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
44
Maana, iliposikika sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, Kitoto kichanga kikaruka kwa furaha.
45
Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana."
46
Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana,
47
na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
48
Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
49
Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea maku, Na jina lake ni takatifu.
50
Na rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mtii yeye.
51
Amefanya nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
52
Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
53
Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54
Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55
(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele."
56
Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
57
Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
58
Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
59
Sasa ilitokea siku ya nane kwamba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, "Zakaria," kwa kuzingatia jina la baba yake,
60
Lakini mama yake akajibu na kusema, "Hapana; ataitwa Yohana."
61
Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili."
62
Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
63
Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, "Jina lake ni Yohana." Wote wakashangazwa na hili.
64
Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
65
Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.
66
Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, " Mtoto huyu kuwa wa namna gani?" Kwasababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
67
Baba yake Zakaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
68
"Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
69
Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
70
kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
71
Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72
Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
73
kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
74
Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu.
75
katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
76
Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
77
kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.
78
Hili litatokea kwa sababu ya huruma ya Mungu wetu, sababu ambayo jua tokea juu litatujia,
79
kuangaza kwao wakaao gizani na katika uvuli wa mauti. Atafanya hivi kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani."
80
Sasa, yule mtoto akakua na kuwa mwenye nguvu rohoni na alikaa nyikani mpaka siku ya kujitokeza kwake kwa Israeli.