1
Hii ndiyo sheria ya sadaka ya hatia. Kwa sababu hiyo ni sadaka takatifu sana.
2
Ni lazima waichinje sadaka ya hatia mahali panapostali kuchinjwa, na ni lazima watainyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
3
Mafuta yote yaliyomo ndani yake yataondolewa: mafuta ya mkiani, mafuta yaliyo sehamu za ndani,
4
zile figo mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake, yaliyo karibu na kiuno, na yanayofunika ini—nyama hii yote lazima iondolewe pamoja na hizo figo.
5
Kuhani ataviteketeza vipande hivi juu ya madhabahu viwe dhabihu iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia
6
Kila mwanaume miongoni mwa familia ya kuhani anaweza kula sehemu ya sadaka hii. Lakini ni lazima iliwe ndani ya mahali patakatifu kwa sababu ni takatifu sana.
7
Nayo sadaka ya dhambi ni kama ilivyo sadaka ya hatia. Ni sheria ile ile hutumika kwa zote mbili. Zote ni mali ya kuhani azitumiaye kufanya upatanisho.
8
Kuhani atoaye sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuchukua ngozi ya sadaka hiyo kwa ajili yake mwenyewe.
9
Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
10
Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Aroni kwa usawa.
11
Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahweh.
12
Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahweh, basi ataitoa pamoja na dhabihu ya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.
13
Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.
14
Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahweh. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.
15
Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.
16
Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.
17
Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.
18
Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi mwenyewe yake.
19
Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.
20
Hata hivyo, mtu najisi anayekula nyama kutoka kwenye dhabihu ya matoleo ya amani ambayo ni ya Yahweh yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
21
Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilicho najisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliyenajisi, au wa kitu fulani kilichonajisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahweh, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
22
Kisha Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
23
"Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
24
Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
25
Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
26
Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
27
Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'"
28
Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
29
"Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
30
Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
31
Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
32
Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.
33
Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Haroni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.
34
Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Haroni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.
35
Huu ndiyo mgao wa Haroni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahweh katika kazi ya kuhani.
36
Huu ndio mgao ambao Yahweh aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.
37
Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,
38
ni sheria ambazo Yahweh alizitoa kwa Musa kwenye Mlima Sinai siku aliyowaamru watu wa Israeli kutoa dhabihu zao kwa Yahweh katika jangwa la Sinai.'"