1
Yahweh akamwambia Musa,
2
"Zungumza na Haroni na wanawe, na watu wote wa Israeli. Waambie mambo ambayo ameamru Yahweh:
3
Mtu yeyote wa Isreli anayeua fahali au mwana—kondoo au mbuzi kambini, au amuuaye nje ya kambi, ili kumtoa dhabihu—
4
kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahweh mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mabali kutoka miongoni mwa watu wake.
5
Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.
6
Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahweh.
7
Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
8
Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
9
na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
10
Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
11
Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai
12
Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.
13
Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi.
14
Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
15
Mtu yeyote alaye mnyama aliyekufa au ambaye amelaruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.
16
Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake".