1
"Njoo, turudi kwa Bwana. Kwa maana ametuvunja vipande vipande, lakini atatuponya; ametujeruhi, lakini atatufunga majeraha yetu.
2
Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, na tutaishi mbele yake.
3
Nasi tumjue Bwana; tukaendelee kumjua Bwana. Kuja kwake ni hakika kama asubuhi; atakuja kwetu kama mvua, kama mvua ya vuli ambayo huinyeshea ardhi."
4
Efraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
5
Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu. Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza.
6
Kwa maana natamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
7
Kama Adamu wamevunja agano; hawakuwa waaminifu kwangu.
8
Gileadi ni jiji la wahalifu wenye miguu ya damu.
9
Kama makundi ya wanyang'anyi wanaomngojea mtu, hivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu; wamefanya uhalifu wa aibu.
10
Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo baya; Uzinzi wa Efraimu ukopale, na Israeli ametiwa unajisi.
11
Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa, nitakaporudisha urithi wa watu wangu.