Sura 34

1 Yahweh akamwabia Musa, "Kata mbao mbili za mawe kama zile za awali. Nitaandika kwenye hizi mbao za mawe maneno yaliyo kuwa kwenye mbao za mawe za mwanzo, mbao za mawe ulizo zivunja. 2 Kuwa tayari asubuhi na uje Mlimani Sinai, na uje mbele zangu juu ya mlima. 3 Hakuna atakaye kuja nawe. Usiruhusu mtu yeyote aonekane popote kwenye mlima. Hakuna kundi la mifugo wanao ruhusiwa hata kula mbele ya mlima." 4 Hivyo Musa akakata mbao mbili za mawe kama za mwanzo, na akaamka asubuhi mapema na kwenda juu ya Mlima Sinai, kama Yahweh alivyo muelekeza. Musa alibeba mbao za mawe mikononi mwake. 5 Yahweh akaja chini katika wingu na akasimama mbele za Musa, na akatamka jina "Yahweh." 6 Yahweh akapita kwake na kukiri, "Yahweh, Yahweh, Mungu ni wa rehema na wa neema, sio mwepesi wa hasira, na anadumu katika uwaminifu wa agano na uadilifu, 7 ukishika uaminifu wa agano kwa vizazi maelfu, ukisamehe maasi, makosa, na dhambi. Lakini hamsafishi mwenye hatia. Ataleta adhabu ya dhambi za baba kwa watoto wao na watoto wa watoto wao, kwa kizazi cha tatu na hadi cha nne." 8 Musa haraka akainamisha kichwa chake kwenye ardhi na kuabudu. 9 Kisha akasema, "Kama sasa nimepata upendeleo machoni pako, Bwana wangu, tafadhali nenda pamoja nasi, kwa kuwa hawa watu ni wakorofi. Samehe maasi yetu na dhambi zetu, na utuchukue kama urithi wako." 10 Yahweh akasema, "Ona, ninakaribia kufanya agano. Mbele za watu wako, nitafanya maajabu ambayo hayajawai kufanyiwa duniani kote wala kwenye taifa lote. Watu wote miongoni mwako wataona matendo yangu, kwa kuwa ni kitu cha hofu ninacho fanya kwako. 11 Tii amri zangu leo. Ninawaondoa mbele yako Waamori, Wakanani, Wahivi, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi. 12 Kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi unayo kwenda, au wata kuwa mtego kwako. 13 Badala yake, lazima uvunje madhabahu zao, ponda nguzo zao za mawe, na kukata nguzo zao za Ashera. 14 Kwa kuwa wewe haupaswi kumuabudu mungu mwingine, maana Yahweh, ambaye jina lake ni wivu, ni Mungu wa wivu. 15 Hivyo kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi, kwa kuwa wanajifanyia ukahaba kwa miungu yao, na wanatoa dhabihu kwa miungu yao. Kisha mmoja wao atakukaribisha na wewe utakula baadhi ya dhabihu zake, 16 na kisha utachukua baadhi ya mabinti zake kwa wanao, na mabinti wake watafanya ukahaba kwa miungu yao, na watafanya wanao kufanya ukahaba kwa miungu yao. 17 Usifanye Miungu ya chuma ya kuyayusha. 18 Laziam ushike Sherehe ya Mkate Usiotiwa chachu. Kama nilivyo kuamuru, lazima ule mkate usio na hamira kwa siku saba kwa muda uliotengwa wa mwezi wa Abibu, maana nikatika mwezi wa Abibu ulitoka Misri. 19 Wazaliwa wote ni mwangu ,hata mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo, yote ya ng'ombe na kondoo. 20 Lazima umnunue tena mzaliwa kwanza wa punda kwa kondoo, lakini usipo mnunua tena, kisha uivunje shingo yake. Lazima ununue tena wazaliwa wa kwanza wote wa wanao. Hakuna hata mmoja atakaye kuja kwangu mikono mitupu. 21 Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Hata wakati wa kilimo na wa mavuno, lazima upumzike. 22 Lazima uadhimishe Sherehe ya Majuma kwa mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano, na lazima uadhimishe Sherehe ya Makusanyo ya mwisho wa mwaka. 23 Mara tatu kwa mwaka wanaume wenu wote watajitokeza kwa Bwana Yahweh, Mungu wa Israeli. 24 Kwa kuwa nitaondoa mataifa mbele yenu na kutanua mipaka. Hakuna atakaye tamani kuwa na ardhi yenu kama yao utakapotoka mbele za Yahweh mara tatu kwa mwaka. 25 Hautatoa damu ya dhabihu yangu na hamira yeyote, wala nyama yeyote kutoka dhabihu za Sherehe ya Pasaka kubaki hadi asubui. 26 Lazima ulete matunda ya kwanza yalio bora kutoka nyumbani kwako. Usimchemshe mbuzi mtoto katika maziwa ya mama yake." 27 Yahweh akamwabia Musa, "Andika chini haya maneno, kwa kuwa nimejiahidi haya maneno niliyo yasema, na nimefanya agano kwako na Israeli." 28 Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi. 29 Musa aliposhuka chini ya Mlima Sinai na mbao mbili za agano za ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa ngozi ya uso wake ilikuwa ina'ngaa akizungumza na Mungu. 30 Wakati Haruni na Waisraeli walipo muona Musa, ngozi ya uso wake ilikuwa inang'aa, na waliogopa kuja karibu naye. 31 Lakini Musa aliwaita, na Haruni na viongozi wa jamii wakaja kwake. Kisha Musa akasema nao. 32 Baada ya haya, watu wote wa Israeli wakaja kwa Musa, na akawambia amri zote Yahweh alizo mpa katika Mlima Sinai. 33 Musa alipomaliza kuzungumza nao, alifunika uso wake kwa kitambaa. 34 Wakati Musa alipoenda mbele za Yahweh kusema naye, aliondoa kitambaa, hadi alipo toka. Alipo toka, aliwaambia Waisraeli alicho amriwa kusema. 35 Waisraeli walipomuona Musa ana'ngaa uso, alirudisha kitambaa tena usoni mpaka alipokuwa anaenda kuongea na Yahweh.