SURA 1

1 Katika siku za utawala wa Ahasuero (huyu ni Ahasuero aliyetawala toka India hadi Ethiopa, zaidi ya majimbo 127), 2 katika siku hizo Mfalme Ahasuero aliketi katika kiti chake cha utawala katika ngome ya Shushani. 3 mwaka wa tatu wa utawala wake, aliwaandalia sherehe viongozi na watumwa wake wote. Waliohudhuria katika sherehe hiyo walikuwa wakuu wa jeshi la Uajemi na Umedi, watu wenye vyeo, na viongozi wa majimbo. 4 Mfalme akaweka wazi utajiri na utukufu wa ufalme wake na heshima ya ukufu wa ukuu alio upata kwa siku nyingi, kwa siku180. 5 Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo.karamu ilifanyika katika Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme. 6 Behewa la bustani, lilipambwa kwa mapazia meupe ya pamba na urujuani.yalifungwa kwa kamba za kitani safi na zambarau, yakiwa yametundikwa kwa pete za fedha na nguzo za marimari. Kulikuwa na makochi ya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marimari, mawe mekundu na meupe, na ya manjano na meusi. 7 Vinywaji viliandaliwa katika vikombe vya dhahabu. Na kila kikombe kilikuwa ni cha kipekee na kwa sababu ya ukarimu wa mfalme kulikuwa mvinyo mwingi. 8 Mfalme aliwambia wahudumu,watu wagawiwe vinywaji , Maana tayari mfalme alikuwa ametoa agizo kwa watumishi wa ikulu kuwafanyia wageni kulingana na matakwa ya kila mgeni. 9 Wanawake nao walikuwa wamealikwa katika karamu na Malkia Vashiti katika ikulu ya Mfalme Ahusuero. 10 katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme) 11 kumleta Malkia Vashiti akiwa katika mavazi yake ya kimalkia. Akiwa na lengo la kuwaonyesha watu na maakida urembo wake, maana alikuwa mrembo. 12 lakini , Malkia Vashiti alikataa kwenda kama mfalme alivyokuwa amewaagiza viongozi wake. Hivyo, mfalme akakasirika sana; ghadhabu yake ikawaka ndani yake 13 Mfalme akawaendea wenye hekima, waliofahamu nyakati (kwa kuwa huu ndio uliokuwa utaratibu wa mfalme kuhusu wale waliokuwa watalaamu wa sheria na hukumu. 14 Carshena, Shethar, Admatha, Tarshish, Meres, Marsena, na Memucan, majimbo saba ya Uajemi na Umedi walikuwa karibu na mfalme na walikuwa na vyeo vikubwa katika ufalme. 15 Katika kutafsiri nini kifanyike kwa mjibu wa sheria kutokana na mgomo wa Malkia Vashiti dhidi ya agizo la mfalme Ahusiero kwa Malkia Vashiti. 16 Memukani alisema mbele ya Mfalme na mbele ya viongozi, Malkia Vashiti hajamkosea tu mfame ,na wakuu, na watu wote walio katika majimbo ya mfale Ahusiero. 17 kwa kuwa jambo la malkia litafahamika kwa wanawake wote.Itawasababisha kuwatendea waume zao vibaya. Watasema, 'Mfalme Ahusiero Malkia Vashiti hakumtii mme wake, Mfalme Ahusiero alipotaka ahudhurie mbele yake.' 18 Kabla ya siku hii wanawake wa wakuu, wa Uajemi na Umedi walioipata taarifa ya mgomo wa malkia Vashiti ,watawatendea waume zao, viongozi wa mfalme. kutakuwa na ghasia na nyingi hasira. 19 kama ni jambo jema kwa mfalme, ruhusu tangazo litolewe, na iwe katika sheria ya Waajemi na Wamedi, ambao haiwezi kutanguliwa, kwamba Vashiti hatakuja tena mbele za mfalme kama malkia. Nafasi ya Vashiti apewe mwingine ambaye ni bora zaidi ya Vashiti. 20 Tangazo la mfalme litakapotolewa katika ufalme wote, wanawake wote watawaheshimu waume zao, tangu mwenye cheo hadi hasiye na cheo." 21 Ushauri huu ulikuwa mzuri kwa mfalme na wakuu wengine, mfalme akafamya kama Memkani alivyopendekeza. 22 Akatuma barua katika majimbo yote ya mfalme, kwa kilajambo na andiko lake, na watu kwa makabila yao. Aliamuru kwamba kila mme awe msimamizi katika nyumba yake mwenyewe. Tangazo hili lilitolewa katika lungha ya kila mtu katika ufalme.