1
Haya ni maneno ya Mwalimu, mwana wa Daudi na mfalme katika Yerusalemu.
2
Mwalimu asema hivi, "Kama mvuke wa ukungu, kama upepo mwanana katika upepo, kila kitu hutoweka na kuacha maswali mengi.
3
Ni faida gani wanadamu huipata kutoka katika kazi zote wazifanyazo duniani?
4
Kizazi kimoja huenda, na kizazi kingine huja, lakini dunia yabaki milele.
5
Jua huchomoza na jua huzama na kwenda kwa haraka, na kurudi mahali linapochomozea tena.
6
Upepo huvuma kusini na huzunguka kaskazini, na mara zote huzunguka katika njia yake na kurudi tena.
7
Mito yote hutiririsha maji bahari, lakini bahari haijai. Mahali mito inakoenda, ndiko inakoenda tena.
8
Kila kitu huwa uchovu, na hakuna yeyote awezae kukielezea. Jicho halishibina kile linachokiona, wala sikio haliriziki na kile linachosikia.
9
Chochote kilichopo ndicho kitakachokuwepo, kila kilichofanyika ndicho kitakachofanyika. Hakuna jipya chini ya dunia.
10
Je kuna jambo lolote ambalo watu wanaweza kusema, 'Tazama, hili ni jipya'? Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo muda mwingi, wakati uliokuwepo kabla yetu.
11
Hakuna anayeonekana kukumbuka kilichotokea nyakati za zamani. Na mambo yaliyo tokea siku zilizo pita na yale yatakayo tokea siku za mbele nayo hayatakumbukwa."
12
Mimi ni mwalimu, na nimekuwa mfalme juu ya Isareli katika Yerusalemu.
13
Nilitia akili yangu katika kusoma na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachofanywa chini ya mbingu. Hili nalo ni jukumu zito ambalo Mungu amewapa wanadamu kujishughulisha nalo.
14
Nimeona matendo yote ambayo yanafanyika chini ya dunia, na tazama yote ni mvuke ni kujaribu kuuchunga upepo.
15
Palipopinda hapawezi kunyoshwa! Kisicho kuwepo hakiwezi kuhesabiwa!
16
Nimeuambia moyo wangu nikisema, "Tazama, nimepata hekima kubwa kuliko walioishi Yerusalemu kabla yangu. Akili yangu imeona hekima kubwa na ufahamu."
17
nilikusudia moyo wangu kujua hekima na upumbuvu na ujinga. Nikagundua kuwa hili nalo pia lilikuwa ni kujaribu kuuchunga upepo.
18
Kwa kuwa katika wingi wa hekima kuna masumbufu mengi, naye aongezae ujuzi, aongeza masikitiko.