1
Kisha tuligeuka na kuanza safari kuelekea jangwani kwa njia ya Bahari ya Mianzi, kama Yahwe alivyosema nami, tulienda kuzunguka mlima wa Seir kwa siku nyingi.
2
Yahwe alizungumza nami, kusema,
3
Mmeuzunguka mlima huu kwa muda mrefu; geukeni kaskazini.
4
Waamuru watu k,wa kusema, "Mtapita kupitia mpaka wa ndugu zenu, wazao wa Esau, ambao wanaishi Seir; watawaogopa ninyi. Kwa hivyo muwe makini
5
msipigane nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote yao, hapana, hakuna hata vya kutosheleza unyao wa mguu kukanyanga, kwa kuwa nimekwisha mpa Esau Mlima wa Seir kama miliki.
6
Mtanunua chakula kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kula, pia mtanunua maji kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kunywa. Kwa kuwa
7
Yahwe Mungu wenu amewabariki katika kazi za mikono yenu, amejua kutembea kwenu kupitia jangwa hili kuu. Kwa hii miaka arobaini Yahwe Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamjapungukiwa chochote.
8
Basi tulipita karibu na ndugu zetu, wa wazao wa Esau, ambao wanaishi Seir, mbali na barabara la Arabah, kutoka Elathi, na kutoka Ezioni Geber. Na tuligeuka na kupita karibu na jangwa la Moabu.
9
Yahweh aliniambia mimi,'Usiisumbue Moabu, na usipigane nao katika vita. Kwa kuwa sitakupa nchi yake kwa miliki yako, kwa sababu nimewapa Ar wazao wa Lot, kuwa miliki yao'.
10
(Hapo awali waliishi Waemi, watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Waanaki;
11
hawa pia wanafikiriwa kuwa Rephaimu, kama Waanaki, lakini Wamoabi huwaita Waemi.
12
Wahori pia waliishi hapo awali Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafuata. Waliwaharibu kutoka mbele yao na kuishi katika eneo lao, kama Israeli ilivyofanya kwa nchi ya umiliki wake ambayo Yahwe aliwapa.)
13
"Sasa inuka na uende kwenye kijito cha Zeredi". Kwa hivyo tulienda kwenye kijito cha Zeredi.
14
Sasa tangu siku ambapo tulikuja kutoka Kadesh Barnea mpaka tukavuka kijito cha Zeredi, ilikuwa miaka thelathini na nane. Ilikuwa kwa wakati huo kizazi chote cha watu waliofaa kupigana walikuwa wamekwisha ondoka kwa watu, kama Yahwe alivyokuwa ameapa kwao.
15
Zaidi ya yote, mkono wa Yahwe ulikuwa kinyume na kizazi hicho ili kuweza kuwaangamiza kutoka kwa watu mpaka walipoondoka.
16
Basi ilitokea, wakati watu wote waliofaa kwa kupigana walikuwa wamekufa, na kutoweka miongoni mwa watu,
17
kwamba Yahwe alizungumza nami, kusema,
18
Leo mtavuka Ar, mpaka wa Moabu.
19
Wakati mtakapofika karibu na mkabala wa watu wa Ammoni, msiwasumbue au kupigana nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote ya watu wa Ammoni kama miliki, kwa sababu nimekwisha wapa wazao wa Lutu kama miliki".
20
(Hiyo tena ilifikiriwa kuwa nchi ya Rephaimu. Warephaimu waliishi hapo awali-lakini Wammonites wanawaita Zamzummim,
21
watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Anakim. Lakini Yahwe aliwaharibu mbele ya Wammonites na waliwafuata na kuishi katika maeneo yao.
22
Yahwe huyu pia alifanya watu wa Esau ambao wanaishi Seiri, wakati alipowangamiza Wahori kutoka mbele yao, na wazao wa Esau waliwafuata na waliishi katika maeneno yao mpaka leo.
23
Na Waavi, walioishi katika vijiji vya mbali ya Gaza, Wakaftori, ambao wanatokana na Kaftori, waliwangamiza na kuishi katika maeneo yao.)
24
Sasa inuka, nenda njia yako na uvuke bonde la Arnoni, tazama, nimekupa mkononi mwako Sihoni ya Amorite, mfalme wa Heshboni, na nchi yake. Anza kuimiliki na pigana naye katika vita.
25
Leo nitaanza kuweka woga na hofu yenu kwa watu ambao wako chini ya anga lote, watasikia habari kuhusu ninyi na watatetemeka na kuwa na shida kwa sababu yenu'.
26
Nilituma wajumbe toka jangwa la Kedemothi kuelekea Sihoni, mfalme wa Heshbon, pamoja na maneno ya amani, kusema,
27
Hebu nipite katika nchi yako; nitapita kwenye barabara kuu, sitageuka mkono wa kulia wala kushoto.
28
Mtaniuzia mimi chakula kwa pesa, ili kwamba niweze kula, nipe maji kwa pesa, ili kwamba niweze kunywa, peke niruhusu kupitia kwa miguu yangu,
29
kama wazao wa Esau wanaoishi Seiri, na Moabu wanaoishi Ari, walifanya kwangu, mpaka nivuke Yordani ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi'.
30
Lakini Sihon, mfalme wa Heshbon, asingeturuhusu kupitia kwake; kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ameifanya ngumu akili yake na kufanya moyo wake kuwa ukaidi, ili kwamba aweze kumshinda kwa nguvu zake, ambayo amekwisha kufanya leo.
31
Yahwe alisema kwangu, "tazama, Nimeanza kumuokoa Sihoni na nchi yake mbele yako; kuanza kuimiliki, ili kusudi muweze kumiliki nchi yake.
32
Kisha Sihon alikuja dhidi yetu, yeye na watu wote wake, kupigana huko Jahazi.
33
Yahwe Mungu wetu alimtoa kwetu na tulimshinda, tulimpiga mpaka kufa, watoto wake, na watu wake wote.
34
Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo na kuharibu kabisa kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo; hatukuacha aliyenusurika.
35
Ng'ombe peke tulichukua kama mateka kwa ajili yetu, sambamba na mateka ya miji tuliochukua.
36
Kutoka Aroer, ambayo iko kwenye ukingo wa bonde la Arnoni, na kutoka kwenye mji ambao uko bondeni, yote kwa njia ya kuelekea Galeadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kwetu. Yahwe Mungu wetu alitupa ushindi dhidi ya maadui zetu mbele yetu.
37
Ilikuwa nchi ya wazao wa Ammoni peke yake ambayo hamkuingia, sambamba na sehemu zote za mto Jabboki, na miji ya nchi ya milima- popote pale Yahwe Mungu wetu ametukataza sisi kwenda.