1
Kuhani mkuu akasema,"mambo haya ni ya kweli"?
2
Stephano akasema, "Ndugu na baba zangu, nisikilizeni mimi: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu wakati alipokuwa Mesopotamia, kabla hajaishi Harani,'
3
alimwambia,' Ondoka katika nchi yako na jamaa zako na uende katika nchi nitakayokuonyesha'.
4
Kisha akaondoka katika nchi ya Ukaldayo akaishi Harani, kutoka hapo, baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta kwenye nchi hii, wanayoishi sasa.
5
Hakumpa chochote kama urithi wake, hapakuwa na sehemu hata ya kuweka mguu. Lakini Abrahamu aliahidiwa hata kabla hajapata mtoto kuwa atapewa nchi yake miliki yake na uzao wake.
6
Mungu alikuwa akinena naye namna hii, ya kwamba wazao wake wangeishi kwa muda katika nchi ya ugeni, na kwamba wenyeji wa pale wangewaleta utumwani na kuwanyanyasa kwa miaka mia nne.
7
' Na Mungu akasema, nitalihukumu taifa ambalo litawafanya watumwa, 'na baada ya hapo watatoka na kuniabudu katika mahali hapa.'
8
Basi Mungu akampa Abrahamu agano la tohara, hivyo Abrahamu akawa baba wa Isaka akamtahiri siku ya nane; Isaka akawa baba wa Yakobo, na Yakobo akawa baba wa mababa zetu kumi na wawili.
9
Kwa sababu mababa zetu wakamwonea wivu Yusufu walimuuza katika nchi ya Misri, lakini Mungu alikuwa pamoja naye,
10
na akamwokoa katika dhiki yake yote, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao mfalme wa Misri. Farao akamfanya awe mtawala juu ya Misri na juu ya nyumba yake yote.
11
Basi kukawa na njaa na dhiki kuu katika nchi ya Misri na Kanani, na baba zetu hawakuweza kupata chakula.
12
Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka Misri, aliwatuma baba zetu kwa safari ya kwanza.
13
Kwa safari ya pili Yusufu alijitambulisha kwa kaka zake, na familia ya Yusufu ikajulikana kwa Farao.
14
Yusufu aliwatuma ndugu zake kwenda kumkaribisha Yakobo baba yao aje Misri, pamoja na jamaa yake yote, jumla ya watu sabini na watano.
15
Hivyo Yakobo akashuka Misri; kisha akafa yeye pamoja na baba zetu.
16
Wakabebwa hata Shekemu wakazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alilinunua kwa vipande vya fedha kutoka kwa wana wa Hamori huko Shekemu.
17
Wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimwahidi Abrahamu ulipokaribia, watu walikua na kuongezeka huko Misri,
18
mpaka mfalme mwingine alipoinuka juu ya Misri, mfalme ambaye hakujua kuhusu Yusufu.
19
Huyo mfalme mwingine aliwalaghai watu wetu na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwalazimisha kuwatoa watoto wachanga waliozaliwa ili wasiachwe hai.
20
Kwa wakati huo Musa alikuwa amezaliwa; alikuwa Mzuri sana mbele za Mungu na kwa miezi mitatu alikuwa akilelewa kwenye nyumba ya baba yake.
21
Alipokuwa ametupwa nje, Binti ya Farao alimchukua akamlea kama mwanawe. .
22
Musa alielimishwa elimu yote ya kimisri na alikuwa Mwenye nguvu kwa maneno na MATENDO yake.
23
Lakini baada ya kutimiza miaka arobaini, ikamjia katika moyo wake kuwatembelea ndugu zake, wana wa Israeli.
24
Alipomwona Mwisraeli akitendewa mabaya, Musa alimtetea na kulipiza kisasi aliyekuwa akimwonea kwa kumpiga Mmisiri:
25
akifikiri kuwa ndugu zake watafahamu kwamba Mungu kwa mkono wake, alikuwa akiwapa wokovu, lakini hawakuelewa.
26
Siku iliyofuata (aliwatokea) baadhi ya Waisraeli waliokuwa wakigombana, akajaribu kuwapatanisha kusema, Enyi wanaume, Nyie ni ndugu; kwanini mnakoseana ninyi kwa ninyi?
27
Lakini aliyekuwa amemkosea Jira I yake akamsukumia mbali, na kusema .... Nani kakuteua kuwa mtawala na hakimu juu yetu?
28
Wewe unataka kuniua, kama ulivyomuua mmisri jana?"
29
Musa alikimbia baada ya kusikia hivyo; akawa mgeni katika nchi ya Midiani, ambapo akawa baba wa wana wawili.
30
Baada ya miaka arobaini kupita, malaika akamtokea katika jangwa la mlima Sinai, katika mwali wa moto ndani ya kichaka.
31
Wakati Musa alipoona moto, alishangaa na kustaajabia kile alichokiona, na alipojaribu kukisogelea ili kukitazama, sauti ya Bwana ikamjia Ikisema,
32
'Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Yakobo'. Musa alitetemeka na hakuthubutu kuangalia.
33
Bwana akamwambia, 'Vua viatu vyako, sehemu uliposimama ni mahali patakatifu.
34
Hakika nimeona mateso ya watu wangu walioko Misri; Nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka ili niwaokoe; sasa njoo, nitakutuma wewe Misri.'
35
Huyo Musa ambaye walimkataa, wakati waliposema, 'nani kakuteua kuwa mtawala na mwamuzi wetu?'- alikuwa ndiye ambaye Mungu alimtuma awe mtawala na mkombozi. Mungu alimtuma kwa mkono wa malaika ambaye alimtokea Musa kichakani.
36
Musa aliwaongoza kutoka Misri baada ya kufanya miujiza na ishara katika Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa kipindi cha miaka arobaini.
37
Ni Musa yule yule aliyewaambia watu wa Isiraeli kuwa, 'Mungu atawainulieni nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu, nabii kama mimi'.
38
Huyu ni mtu ambaye alikuwa katika mkutano jangwani na malaika ambaye aliongea naye katika mlima Sinai. Huyu ndiye mtu ambaye alikuwa na baba zetu, huyu ni mtu ambaye alipokea neno lililo hai na kutupatia sisi.
39
Lakini baba zetu walikataa kumtii; walimsukumia mbali nao, na katika mioyo yao waligeuka kurudi Misri.
40
Katika kipindi hicho walimwambia Haruni.'tutengenezee miungu itakayotuongoza. Kwakua huyu Musa, aliyekuwa akituongoza kutoka katika nchi ya Misri, hatujui kilichompata.'
41
Hivyo walitengeneza ndama kwa siku hizo na wakatoa sadaka kwa hiyo sananmu na wakafurahi kwa sababu ya kazi ya mikono yao.
42
Lakini Mungu aliwageuka na kuwaacha waabudu nyota za angani, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha manabii, 'Je Mmenitolea mimi sadaka za wanyama mliowachinja jangwani kwa muda wa miaka arobaini, nyumba ya Israeli?
43
Mmekubali hema ya kukutania ya Moleki na nyota ya Mungu refani, na sanamu mlizozitengeneza kuziabudu: na nitawapeleka mbali zaidi ya Babeli.'
44
Baba zetu walikuwa na hema ya kukutania ya ushuhuda jangwani, kama Mungu alivyoamuru alipoongea na Musa, kwamba ilimpasa aitengeneze mfano wa muundo ule aliouona.
45
Baadaye, baba zetu, chini ya Yoshua, walilipokea lile hema na kuilileta pamonja nao walipomiliki nchi. Mungu alichukua nchi ile kutoka kwa mataifa na kuwafukuza mbele ya uso wa baba zetu. Hema lilibaki katika nchi hadi wakati wa Daudi,
46
ambaye alipata kibali machoni pa Mungu,' na akaomba kutafuta makao kwa ajaili ya nyumba ya Yakobo.
47
Lakini ni Sulemani aliyejenga nyumba ya Mungu.
48
Hata hivyo Aliye Juu sana huwa haishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono; kama nabii anavyosema,
49
Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni sehemu ya kuwekea miguu yangu. Nyumba ya aina gani mtanijengea?, asema Bwana: au ni wapi sehemu yangu ya kupumzikia?
50
Mkono wangu haukufanya hivi vyote?'
51
Enyi watu wenye shingo ngumu msiotahiriwa mioyo na masikio, kila mara mnampinga Roho Mtakatifu,' mnatenda kama baba zenu walivyotenda.
52
Ni nabii yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumtesa?. Waliwaua manabii wote waliotokea kabla ya ujio wa yule mwenye Haki,'na sasa mmekuwa wasaliti na wauaji wake pia,
53
enyi watu mliopokea sheria ile iliyoagizwa na malaika lakini hamkuishika."
54
Kisha wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya, walighadhabika sana mioyoni mwao, na wakamsagia meno Stefano.
55
Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni kwa makini na akauona utukufu wa Mungu,' na kumwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
56
Stefano akasema, "Angalia, ninaona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adam amesimama mkono wa kuume wa Mungu."
57
Kwa hili wajumbe wa baraza waliziba masikio Yao na kupiga kelele kwa Sauti ya juu na kumvamia kwa kusudi moja.
58
kwa nguvu wakamtupa nje ya mji na wakaanza kumpiga mawe: na mashahidi wakavua nguo zao za nje na kuweka chini karibu na miguu ya kijana aliyeitwa Sauli.
59
Walipokuwa wakimpiga mawe Stefano, aliendelea kumwita Bwana na kusema, "Bwana Yesu, pokea roho yangu,".
60
Alipiga magoti akilia kwa sauti kubwa akiita, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii". Aliposema haya, akakata roho.