2 Mambo Ya Nyakati
Sura 9
1
Malkia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa
2
Sulemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Sulemani akamjibu maswali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Sulemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
3
Malkia wa Sheba alipoiona hekima ya Sulemani na ikulu aliyokuwa amejenga,
4
chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.
5
Akasema kwa mfalme, "Ni kweli, taarifa nilioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.
6
Sikuamini nilichokisikia mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.
7
Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. (Baadhi ya maandiko yanasema, "Wambarikiwa wake zako", ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10: 8).
8
Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako anaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.
9
Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vitu vya thamani. Sulemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki ambacho alipewa na malkia wa Sheba.
10
Watumishi wa Hiramu na mfalme Sulemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali,, na vito vya thamani.
11
Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Sulemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.
12
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Sulemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na watumishi wake.
13
Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Sulemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,
14
nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Wafalme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Sulemani dhahabu na fedha.
15
Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.
16
Pia akatengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyopigwa. Minas tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.
17
Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.
18
Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiti cha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.
19
Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.
20
Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Sulemani.
21
Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.
22
Kwa hiyo Mfalme Sulemani aliawazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.
23
Dunia yote waliutafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
24
Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.
25
Sulemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
26
Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.
27
Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya aridhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.
28
Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Sulemani.
29
30
31
Kwa mambo mengine kuhusu Sulemani, mwanzo na mwisho, hayajandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati? 30 Sulemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.31 Akalala na babu zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.