Sura 19

1 Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko. 2 Paulo akawaambia, "Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?" Wakamwambia, "apana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu." 3 Paul alisema, "Sasa ninyi mlibatizwaje?" Wakasema, "Katika ubatizo wa Yohana. 4 Basi Paulo akajibu, "Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu." 5 Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. 7 Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili. 8 Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwashawishi watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu. 9 Lakini Wayahudi wengine waliokuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea kila siku katika ukumbi wa Tirano. 10 Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani. 11 Mungu alikuwa akifanya miunjiza kwa mikono ya Paulo, 12 kwamba hata wagonjwa waliponywa, na pepo wachafu waliwatoka, wakati walipochukua vitambaa na nguo zilizokuwa zimeguza mwilini wa Paulo. 13 Lakini palikuwepo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu ili wawe na nguvu juu ya pepo chafu. Wakisema, "Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri." 14 Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi,aliyeitwa Skeva. 15 Roho mchafu akawajibu, "Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? " 16 Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa. 17 Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa. 18 Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na kukiri matendo mabaya waliyoyafanya. 19 Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha. 20 Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana na katika nguvu. 21 Sasa baada  ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso,Paulo akaamua kwa mwongozo wa Roho kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, "Baada ya kuweko huko, yanipasa kuiona Rumi pia." 22 Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda. 23 Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia. 24 Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu wakike aitwaye Artemis, alileta biashara kubwa kwa mafundi. 25 Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, "Enyi watu, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi. 26 Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema miungu iliyo tengenezwa kwa mikono sio miungu. 27 Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke Artemi anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu 28 Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, "Diana wa Waefeso ni mkuu." 29 Mji wote ukajaa ghasia, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia. 30 Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia. 31 Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo. 32 Baadhi ya watu walikuwa wakisema kitu hiki na wengine jambo lile, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja. 33 Wayahudi wakamleta Aleksanda nje ya umati wa watu na kumuweka juu mbele ya watu. Aleksanda akatoa ishara kwa mkono wake kutoa maelezo kwa watu. 34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, "Artemis ni mkuu wa Wafeso." 35 Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, 'Enyi watu  wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Artemi mkuu na ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni? 36 Kuona basi kwamba mambo haya hayapingiki,tunapaswa kuwa na utulifu na msifanye chochote kwa haraka. 37 Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu wa kike. 38 Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri. 39 Lakini kama wewe watafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali. 40 Kwa kuwa tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza. Baada ya kusema haya, aliutawanya makutano.