1 Ikatokea ndani ya Ikonio kwamba Paulo na Barnaba waliingia pamoja ndani ya sinagogi la Wayahudi na kuongea namna ambavyo kundi kubwa la watu Wayahudi na Wayunani waliamini. 2 Lakini wayahudi wasiotii waliwachochea akili watu wa mataifa na kuwafanya kuwa wabaya dhidi kati ya mandugu. 3 Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku wakitoa ushahidi kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya hivi kwa kutoa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba. 4 Lakini watu wa mji waligawanyika: baadhi walikuwa pamoja na Wayahudi, na baadhi pamoja na mitume. 5 Wakati watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na viongozi wao walipojaribu kuwatendea mabaya na kuwaponda mawe, 6 lakini walipotambua hilo, wakakimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale, 7 ambako waliendelea kutangaza injili. 8 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hakuwahi kutembea. 9 Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa. 10 Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, "Simama kwa miguu yako." Na yule mtu alisimama juu na kuanza kutembea. 11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, "miungu imetushukia kwa namna ya binadamu." 12 Walimwita Barnaba "Zeu," na Paulo "Herme," kwa sababu alikuwa msemaji mkuu. 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka. 14 Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka wakaenda nje kwenye umati, wakiliana kusema, 15 "Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama zenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo. 16 Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe. 17 Lakini bado, hakuacha kama hana shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha" 18 Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka. 19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburura hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa. 20 Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, wakaingia mjini. Siku ya pili,walienda Derbe na Barnaba. 21 Baada ya kutangaza injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikoniamu, na hadi Antiokia. 22 Waliendelea kuimarisha nafsi za wanafunzi na kuwatia moyo kuendelea katika imani, akasema, "Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia mateso mengi." 23 Walipo wateua wazee kwa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini. 24 Kisha walipita katika Pisidia na wakafika Pamfilia. 25 Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia. 26 Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha. 27 Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kanisa pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa. 28 Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.