1
Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, "Inuka na uende pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu BWANA ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba."
2
Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba.
3
Ikafika kama mwishoni mwa miaka saba yule mwanamke akarudi kutoka kwenye ile nchi ya Wafilisti, na kwenda kwa mfalme kumuomba nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.
4
Basi mfalme alikuwa anaongea na Gehazi yule mtumishi wa Mungu, akisema, "Tafadhali niambie yale mambo makubwa ambayo Elisha ameyafanya."
5
Basi alipokuwa akimwambia yule mfalme jinsi gani Elisha alivyomfufua yule mtoto aliyekufa, huyo mwanamke ambaye mtoto wake aliyekuwa amefufuliwa akaja kumuomba yule mfalme kwa ajili ya nyumba yake na nchi yake. Gehazi akasema, "Bwana wangu, mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, na huyu ndiye mtoto wake, ambaye Elisha amemfufua."
6
Wakati yule mfalme alipomuuliza yule mwanamke kuhusu mtoto wake, alimwelezea yule mfalme. Ndipo mfalme akamwagizia akida, akisema, "Mrudishie vyote vilivyokuwa vyake na mavuno yake yote ya mashamba tangu siku alipoondoka hadi sasa."
7
Elisha akaja Dameski ambako Ben Hadadi yule mfalme wa Shamu alikuwa anaumwa. Yule mfalme aliambiwa, "Yule mtu wa Mungu amekuja hapa."
8
Mfalme akamwambia Hazaeli, "Chukua zawadi kwenye mkono wako na uende ukakutane na mtu wa Mungu, na ukazungumze na BWANA kupitia yeye, ukisema, "Je nitapona huu ugonjwa wangu?"
9
Basi Hazaeli akaenda kuonana naye na kuchukua zawadi zake za kila kitu kizuri cha
Dameski, akabeba ngamia arobaini. Hivyo Hazaeli akaja na kusimama mbele ya Elisha na kusema, "Mtoto wako Ben Hadadi mfalme wa Shamu amenituma kwako, kusema, "Je nitapona huu ugonjwa?"
10
Elisha akamwambia, "Nenda, kwa Ben Hadadi, 'ukamwambie Utapona hakika,' lakini BWANA amenionyesha kwamba atakufa hakika."
11
Basi Elisha akamkazia macho Hazaeli hadi alipojisikia aibu, na yule mtu wa Mungu akalia machozi.
12
Hazaeli akauliza, kwa nini unalia, bwana wangu?" Akajibu, "Kwa sababu najua uovu ambao utakaoufanya kwa watu wa Israeli. Utazichoma moto ngome zao kwa moto, na utawaua vijana wao kwa upanga, kuwaseta vipande vipande watoto wao wachanga, na kuwapasua mimba zao wanawake wenye mimba."
13
Hazaeli akajibu, Ni nani mtumwa wako, ambaye atafanya jambo hili kubwa? Yeye ni mbwa tu." Elisha akajibu, "BWANA amenionyesha kwamba utakuwa mfalme juu ya Shamu."
14
Ndipo Hazaeli akamwacha Elisha na kuja kwa bwana wake, ambaye alimwambia, "Je Elisha alikwambiaje?" Akajibu, "Ameniambia kwamba utapona bila shaka."
15
Basi siku ya pili yake Hazaeli akachukua tandiko la kitandai na kulichovya kwenye maji, na kulitandaza kwenye uso wa Ben Hadadi hivyo akafa. Basi Hazaeli akawa mfalme katika sehemu yake.
16
Katika mwaka wa kumi na tano wa Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Yehoramu akaanza kutawala. Alikuwa mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Alianza wakati Yehoshafati alikuwa mfalme wa Yuda.
17
Yoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka minane katika Yerusalemu.
18
Yoramu akatembea kwenye njia ya huyo mfalme wa Israeli, kama walivyokuwa wakifanya kwenye nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mke wake, na alifanya uovu machoni pa BWANA.
19
Walakini, kwa sababu ya mtumishi wake Daudi, BWANA hakutaka kuiharibu Yuda, tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao.
20
Katika siku za Yoramu, Edomu akaasi kutoka chini ya mkono wa Yuda, na wakamfanya mfalme juu yao wenyewe.
21
Basi Yoramu akaenda na makamanda wa jeshi na magari ya farasi yote. Ilitokea kwamba akaamka usiku na kushambulia na kuwazunguka Waedomu, waliokuwa wamemzunguka na wale makamanda wa jeshi la magari ya farasi. Ndipo wanajeshi wa Yehoramu wakakimbilia majumbani kwao.
22
Hivyo Edomu aliasi dhidi ya utawala wa Yuda katika siku hizi. Libna pia aliasi katika kipindi hicho hicho.
23
Kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoramu, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
24
Yehoramu akafa na kuzikwa pamoja na baba zake, na akalala pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Ndipo Ahazi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
25
Katika mwaka wa kumi na mbili wa Yehoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
26
Ahazi alikuwa ana umri wa miaka ishirini na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Athalia; alikuwa mtoto wa Omri, mfalme wa Israeli.
27
Ahazia alitembelea katika nyumba ya Ahabu; alifanya yale yaliyo maovu katika uso wa BWANA, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa kuwa Ahazia alikuwa mkwe kwenye nyumba ya Ahabu.
28
Ahazia akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Shamu, katika Ramoth Geleadi. Washami wakamjeruhi Yoramu.
29
Mfalme Yoramu akarudi ili auguzwe huko Yezreeli kwenye yale majeraha ambayo Washami walimpatia huko Rama. Wakati alipopigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Hivyo Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akashuka kwa Yezreeli kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.