1
Wana wa manabii wakamwambia Elisha, "Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.
2
Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi." Elisha akajibu, "Unaweza kwenda mbele."
3
Mmoja wao akasema, "Nenda na watumishi wako tafadhali." Elisha akajibu, "Nitaenda."
4
Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.
5
Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, "La hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!"
6
Basi mtu wa Mungu akasema, "kiliangukia wapi?" Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. akakata kijiti, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
7
Elisha akasema, "Kichukue." Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.
8
Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, "kambi yangu itakuwa sehemu fulani na fulani."
9
Basi huyo mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, akisema, "Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo."
10
Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.
11
Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, "Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?"
12
Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, "Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala."
13
Yule mfalme akajibu, "Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata." Akaambiwa, "Tazama yuko Dothani."
14
Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.
15
Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, "Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?"
16
Elisha akajibu, "Usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao."
17
Elisha akajibu na kusema, "BWANA, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona." Ndipo BWANA alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto
yamemzunguka Elisha!
18
Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa BWANA na kusema, "Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba." Hivyo BWANA akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.
19
Kisha Elisha akawaambia Washami, "Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta." Ndipo akawaongoza kwenda Samaria.
20
Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, "BWANA, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona." BWANA akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.
21
Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, "Baba yangu, niwaue? Niwaue?"
22
Elisha akajibu, "Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao."
23
Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Washami halikurudi kwa muda mrefu katika nchi ya Israeli.
24
Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.
25
Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
26
Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoja akamlilia akisema, "Nisaidie, bwana wangu, mfalme."
27
Akasema, "Kama BWANA hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?"
28
Mfalme akaendelea, "Nini kinakusumbua?" Akajibu, "Huyu mwanamke ameniambia, 'Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wa kwangu kesho.'"
29
Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, "Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake."
30
Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia
31
Kisha akasema, "Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo."
32
Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, "Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivyotumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?"
33
Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, "Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa BWANA. Kwa nini nimsubiri BWANA tena?"