1
Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.
2
Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.
3
Alikuwa amoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya BWANA, kwa muda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.
4
Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta makamanda wamaamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya BWANA. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya BWANA. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.
5
Akawaamuru, akisema, "Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,
6
na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi."
7
Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya BWANA kwa ajili ya mfalme.
8
Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.
9
Hivyo mamia ya makamanda wamaamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.
10
Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa makamanda wamaamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya BWANA.
11
Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.
12
Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpa ushuhuda. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, "Mfalme na aishi!"
13
Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba
ya BWANA
14
Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na wakuu na wapiga baragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, "Uhaini! Uhaini!"
15
Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza makamanda wa jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, "Mtoeni kwenye safu." Atakayemfuata, muueni kwa upanga." Kwa kuwa kuhani alisema, "Msimwache auawe kwenye nyumba ya BWANA."
16
Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.
17
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya BWANA na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa BWANA, na pia kati ya mfalme na watu.
18
Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la BWANA.
19
Yehoyada akawachukua makamanda wa jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya BWANA na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.
20
Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.
21
Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.