1
Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema,
2
"Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amri zake,
3
maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwangalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,
4
na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, 'Kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.'
5
Wewe pia wajua kile Yoabu mwana wa Seruya alichonifanyia, na kile alichowafanyia majemedari wa majeshi ya Israeli, kwa Abina mwana wa Neri, na kwa Amasa mwana wa Yetheri, ambaye alimwua. Alimwaga damu vitani wakati wa amani na kuiweka ile damu kwenye mshipi uliokuwa kiunoni mwake na kwenye vile viatu miguuni mwake.
6
Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani.
7
Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.
8
Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,'
9
Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu, Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini."
10
Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
11
Siku ambazo Daudi alitawala Israeli zilikuwa ni miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
12
Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
13
Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathsheba mama wa Sulemani. Naye akamwuliza, "Je, unakuja kwa amani?" Naye akajibu, "Kwa amani."
14
Kisha akasema, "Nina jambo la kukuambia." Naye akajibu, "Sema."
15
Adoniya akasema, "Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.
16
Sasa nina ombi moja kwako, usinikatalie." Bathsheba akamwambia, "Sema."
17
Naye akamwambia, "Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu."
18
Bathisheba akamwambia, "Vyema sana, nitamwambia mfalme."
19
Kwa hiyo Bathsheba akaenda kumwambia mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akakaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akakaa mkono wa kuume wa mfalme.
20
Ndipo alipomwambia, "Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie." Mfalme, akamjibu, "Mama omba kwa kuwa sitakukatalia."
21
Naye akamwambia, "Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake."
22
Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, "Kwa nini unamwombea Adonia huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?"
23
Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, "Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adonia hajayasema haya kinyume na maisha yake.
24
Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo."
25
Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.
26
Kisha akamwambia Abiathari kuhani, "Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. Unastahili kufa, lakini sitakuua sasa hivi, kwa sababu ulilibeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitaabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata taabu."
27
Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.
28
Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adonia, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu.
29
Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, "Nenda, ukamwue."
30
Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, "Mfalme anasema utoke hemani." Yoabu akamjibu, "Hapana. Nitafia hapa." Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, "Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu."
31
Naye mfalme akamwambia, "Kafanye kama alivyosema. Muue na ukamzike, ili kwamba uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu.
32
BWANA na amrudishie damu yake kichwani kwake, kwa sababu aliwaua wanaume wawili wasio na hatia na wema kuliko yeye na akawaua kwa upanga, Abineri mwana wa Neri, Jemedari wa Jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Jetheri, jemedari wa jeshi la Yuda, bila baba yangu Daudi kujua.
33
Kwa hiyo damu yao na imrudie Yoabu kichwani pake na kwenye vichwa vya uzao wake milele na milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, na nyumba yake, na kwenye kiti chake cha enzi, kuwe na amani ya kudumu kutoka kwa BWANA."
34
Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani.
35
Mfalme akamwinua Benaya mwana wa Yehoyada kuwa juu ya jeshi badala yake, na akamweka Sadoki kuhani kwenye nafasi ya Abiatahari.
36
Kisha Mfalme akatuma watu kumwita Shimei, na akamwambia, "Kajijengee nyumba kwa ajili yako kule Yerusalemu na uishi huko, na usitoke nje ya huo mji na kwenda mahali pengine.
37
Kwa kuwa siku utakayoenda mahali pengine, na kupita bonde la Kidroni, ujue kwa hakika kuwa utakufa. Damu yako itakuwa juu ya kichwa chako."
38
Kwa hiyo Shimei akamwambia mfalme, "Unachosema ni chema. Kama vile mfalme bwana wangu alivyosema, ndivyo ambavyo mtumishi wako atakavyofanya." Kwa hiyo Shimei akaishi Yerusalemu kwa miaka mingi.
39
Lakini mwishoni mwa mwaka wa tatu, watumishi wawili wa Shimei wakakimbilia kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Kwa hiyo wakamwambia Shimei, wakisema, "Tazama, watumishi wako wameenda Gathi."
40
Kisha Shimei akainuka, akapanda punda wake akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumishi wake. Akaenda na akawaleta watumishi wake toka Gathi.
41
Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi na amerudi,
42
mfalme akatuma wito kwa Shimei na kumwambia, "Je, sikukuapisha kwa BWANA na kushuhudia kwako, nikisema, 'Tambua kuwa siku utakayotoka kwenda nje na kwenda mahali popote, hakika utakufa?' Na ukaniambia kuwa unachosema ni chema.
43
Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako kwa BWANA na amri niliyokupa?"
44
Pia mfalme akamwambia Shimei, "Unajua katika moyo wako maovu yote uliyofanya kwa baba yangu Daudi. Kwa hiyo BWANA atakurudishia maovu yako kichwani pako.
45
Lakini Sulemani atabarikiwa na enzi ya Daudi itaimarika mbele ya BWANA milele."
46
Kwa hiyo mfalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada kwenda kumwua Shimei. Kwa hiyo ule utawala ulikuwa mwema kwa mkono wa Sulemani.