Sura 8

1 Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara, 2 Noha, na Rafa. 3 Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi, 4 Abishau, Naamani, Ahoa, 5 Gera, Shefufani, na Huramu. 6 Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati: 7 Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi. 8 Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara. 9 kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu, 10 Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao. 11 Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu. 12 Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi ( ambao walijenga Ono na Lodi pamoja na vijiji vilivyozunguka.) 13 Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya nyumba za baba zao wa walioishi Aijaloni, ambao waliwaondoa wakazi wa Gati. 14 Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15 Zebadia, Aradi, Eda, 16 Mikaeli, Ishipa, na Joha 17 walikuwa wa na wa Beria Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba, 18 Ishimerai, Izilia, na Yobabu walikuwa wana wa Elipaali. 19 Yokimu, Zikri, Zabdi, 20 Elienai, Zilletai, Elieli, 21 Adaia, Beraia, na Shimrati walikuwa wana wa Shimei. 22 Ishipani, Eba, Elieli, 23 Abdoni, Zikri, Hanani, 24 Hanania, Elamu, Antothiya, 25 Ifdeia, na Penueli walikuwa wana wa Shashaki. 26 Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27 Yaareshia, Eliya, na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu. 28 Hawa walikuwa vichwa vya koo- kwa mujibu wa kumbukumbu za koo zao walikuwa vichwa. Walikuwa wanaume wakuu walioishi Yerusalemu. 29 Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni. 30 Mzaliwa wake wa kwanza wa kiume alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Zuri, Kishi, Baali, Nadabu 31 Gedori, Ahio, na Zekari. 32 Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu. 33 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali. 34 Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika. 35 Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi. 36 Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza. 37 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli. 38 Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli. 39 Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu. 40 Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.