1 Daudi akakusanya maafisa wote wa Israeli Yerusalemu: maafisa wa makabila, maafisa wa vitengo walio mtumikia mfalme katika kazi walizo pangiwa, wakuu wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali zote za mfalme na wanawe, na maafisa na wanaume wa mapambano, ukijumuisha wale wenye ujuzi sana. 2 Kisha Daudi mfalme akainuka kwa miguu yake na kusema, "Sikilizeni mimi, kaka zangu na watu wangu. Ilikuwa dhumuni langu kujenga hekalu kwa ajili ya sanduku la agano la Yahweh; stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu, na nimefanya maandalizi kuijenga. 3 Lakini Mungu akaniambia, 'Hautajenga hekalu kwa ajili ya jina la langu, kwasababu wewe ni mwanaume wa vita na umemwaga damu.' 4 Bado Yahweh, Mungu wa Israeli, alinichagua kutoka katika familia ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Amechagua kabila la Yuda kama kiongozi. Katika kabila la Yuda, na nyumba ya baba yangu, kutoka kwa wana wa baba yangu, amenichagua kuwa mfalme wa Israeli. 5 Kutoka kwa wana wengi ambao Yahweh amenipa, amemchagua Sulemani, mwanangu, kuketi katika kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli. 6 Aliniambia, 'Sulemani mwanae atanijengea nyumba yangu na nyuani mwangu, kwa kuwa nimemchagua kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake. 7 Nitaimarisha ufalme wake, akidumu kutii sheria na amri zangu, kama ulivyo siku ya leo.' 8 Kisha sasa, katika macho ya Waisraeli wote, hili kusanyiko la yahweh, na katika uwepo wa Mungu wetu, nyinyi nyote lazima mshike na kufanya amri zote za Yahweh Mungu wenu. Fanyeni hivi ili mmiliki nchi hii nzuri na kuiacha kama urithi kwa uzao wenu baada yenu milele. 9 Kwako wewe, Sulemani mwanangu, mtii Mungu wa baba yako, mtumikie kwa moyo wako wote na roho ya utayari. Fanya hivi kwa sababu yahweh anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu. Ukimtafuta, ataonekana nawe, lakini ukimtelekeza, atakukataa milele. 10 Elewa kuwa Yahweh amekuchagua kulijenga hekalu hili kama patakatifu pake. Uwe hodari na uifanye." 11 Kisha Daudi akamkabidhi Sulemani mwanae mipango ya ukumbi wa hekalu, majengo ya hekalu, vyumba vya hifadhi, vyumba vya juu, vyumba vya ndani, na chumba chenye kifuniko cha upatanisho. 12 Alimpatia mipango aliyo chora ya nyuani kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vyumba vyote vilivyo zunguka, vyumba vya hifadhi katika nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vya Yahweh. 13 Alimpatia masharti kwa vitengo vya makuhani na Walawi, kwa majukumu walio pangiwa kwa utumishi wa nyumba ya Yahweh, na kwa vyombo vyote vinavyo tumika katika nyumba ya Yahweh. 14 Aliamua uzito wa vifaa vyote vya dhahabu kwa kila huduma, uzito wa vifaa vya fedha kwa kila huduma, 15 uzito wa dhahabu wa vifaa vyote vya dhahabu, kuwavinara vya taa na taa za dhahabu, uzito wa dhahabu kwa kila kinara cha taa, uzito wa fedha kwa kila kinara cha fedha, kulingana na matumizi ya kila kinara cha taakatika huduma. 16 Alitoa uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha. 17 Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa uma za nyama, beseni, na vikombe. Alitoa uzito kwa kila bakuli ya dhahabu, na uzito kwa kila bakuli ya fedha. 18 Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya uvumba, na za dhahabu kwa muundo wa gari, makerubi waliye tanda mabawa yao na kufunika sanduku la agano la Yahweh. 19 Daudi akasema, " Nimeweka haya katika maandishi kama Yahweh alivyonielekeza na kunipa kuelewa kuhusu mchoro." 20 Daudi akasema kwa Sulemani mwanae, "Kuwa hodari na mjasiri. Fanya kazi. Usiogope au kufadhai, kwa kuwa Yahweh Mungu, Mungu wangu, yupo nawe. Hatakuacha wala kukutelekeza mpaka kazi ya huduma ya hekalu la Yahweh imekamilika. 21 Ona, hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi kwa huduma katika hekalu la Mungu. Watakuwa nawe, pamoja na wanaume walio tayari na wenye ujuzi, kukusaidia katika kazi na kutenda huduma. Maafisa na watu wote wako tayari kufuata amri zako."