1 Haya ndiyo makundi yawalinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu. 2 Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne, 3 Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba. 4 Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano, 5 Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu. 6 Kwa Shemaia mwanaye walizawa wana walio tawala koo zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mkuu. 7 Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali. 8 Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na jamaa zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu. 9 Meshelemia alikuwa na wana na jamaa, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane. 10 Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (ijapo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi), 11 Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na jamaa walikuwa kumi na tatu kwa idadi. 12 Haya makundi ya walinzi wa lango, sambamb a na viongozi, yalikuwa na majukumu, kama jamaa zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh. 13 Walipiga kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na koo zao, kwa kila lango. 14 Kura ilipo pigwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanaye, mshauri mwenye busara, na kura yake ikatokea kwa lango la kaskazini. 15 Kwa Obedi Edomu alipangiwa lango la kusini, na wanawe walipangiwa nyumba za ghala. 16 Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwenye barabara ya juu. Walinzi walikuwa karibu sana. 17 Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini wanne kwa siku moja, kusini wanne kwa siku moja, na nyumba za ghala jozi mbili. 18 Kwenye nguzo upande wmagharibi wanne kulikuwa na wanne waliosimama kwenye barabara na wawili kwenye nguzo. 19 Haya yalikuwa makundi ya walinzi wa lango waliokuwa uzao wa Kora na Merari. 20 Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh. 21 Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli 22 na wanae Yehieli: Zethamu na Yoeli kaka yake. Walikuwa wamesimamia hazina za nyumba ya Yahweh. 23 Kutoka koo za Amramu, koo za Izhari, koo za Hebroni, na koo za Uzieli: 24 Shebueli uzao wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa hazina. 25 Jamaa zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanawe, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi. 26 Shelomothi na jamaa zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga. 27 Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh. 28 Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na jamaa zake. 29 Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi. 30 Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1, 700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme.Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani. 31 Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa koo, kulingana na orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo mkubwa katika Yazeri ya Gileadi. 32 Yerija alikuwa na ndugu 2, 700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.