1 Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katikati ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu. 2 Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh. 3 Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu. 4 Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli. 5 Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze vinanda na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele. 6 Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu. 7 Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh. 8 Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake. 9 Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu. 10 Jisifuni katika jina lake takatifu; acha mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie. 11 Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote. 12 Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake, 13 enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake. 14 Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote. 15 Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja. 16 Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka. 17 Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele. 18 Alisema, "Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako." 19 Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana, kuwa wageni katika nchi, 20 walitangatanga kutoka taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. 21 Hakumruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao. 22 Alisema, " Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu." 23 Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku. 24 Tangazeni utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote. 25 Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote. 26 Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliyeziumba mbingu. 27 Fahari na ukuu zipo uweponi mwake. Nguvu na furaha zipo mahali pake. 28 Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni Yahweh utukufu na nguvu; 29 Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika fahari ya utakatifu 30 Tetemeka mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika. 31 Mbingu nazifurahi, na dunia ishangilie; na wasema kati ya mataifa, "Yahweh anatawala." 32 Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake. 33 Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia. 34 Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake hudumu milele. 35 Kisha sema, "Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako." 36 Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, "Amina" na wakamsifu Yahweh. 37 Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa. 38 Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango. 39 Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni. 40 Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria. 41 Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwa sababu uaminifu wa agano lake la dumu hatamilele 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango. 43 Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kuwabariki watu wa nyumbani mwake.