Sura 2

1 Kwa kfa nyoonyo mveni muishi, ndugu, kwa ujio weedu kwenu uveekeri wa bure ku. 2 Muishi kwamba lakwooka duleteseka na valedutendea kwa haibu kula filipi, shaali muishi. Kuveere ujasiri katika Ruva ichecha injili ya Ruva hata katika taabu nyiingi. 3 Kwa maana mahusia yedu yefumana na uviishwa, wadha katika ushafu, wadha katika hila. 4 Badala yakwe, sha vile ulekubadilika na Ruva na iaminiwa injili, nakdo durenena. Tunanena, si kwa kuwafurahi vandu, lakini imfurahisha Ruva. Ve eemeni nave echunguza mioyo yedu. 5 Kwa maana duletumia maneno yejipendekesa wakati wooseku, shaali muishi, wala uletumia machecha sha ksingisio kwa tamaa, Ruva ni mshahidi wedu. 6 Wala duletafuta utukufu kwa vanduku, wala ifuma kwenu au kwa vengi. Duvedima idai ipelelezwa sha mtume wa Kristo. 7 Badala yake vahoo kati yenu shaali mama efariji vana vakwe eeveni. 8 Kwa shia i duveekeri na upendo kwenu. Duveekeri radhi ivashirikisha si injili ya Ruva bali pia na maisha yedu duveeni. Kwakfa mleva vapendwa vedu. 9 Kwa kfa ndugu, muikumbwa kasi na taabu sedukio na kwaaya duveekeri duufanya kasi kusudi dutashe mdhemea woose. Wakati sho, dulevahubiria injili ya Ruva. 10 Nyohonyo ni uashahidi, na Ruva pia, ni kwa utakatifu wa namna yonki, haki, na bila dhawama tulivoenda duveeni mbedhe yenu nyomweamini. 11 Vovyo hivyo, muishi ni kwa namna yonki kwa kidha umu wenu, shaali papa ekeri kwa mwana wakwe dulevahimisa na ivaininga moyo duleshuhudia. 12 Kwamba mlepaswa ienda shaali mwito wenu kwa Ruva,shoelevadhaha kweny ufalme na utukufu wakwe. 13 Kwa sababu yohoyo dwamshukuru Ruva pia kidh saa. Kwa kfa saa mlipopokea uika kwedu ujumbe wa Ruva yomleishwa, mleambilia, si sha checha la wanadamu. Badadha yakwe, mleambilia sha dhoi ikeri, checha la Ruva. Ni ichechali ambalo lerunda kasi kati yenu nyomweamini. 14 Kwa hiyo nyohoyo,ndugu,mve vandu veiga makanisa yab Ruva yoyekeri katika uyahudi katika kristo Yesu. Kwa kuwa nyohonyo pia mleteseka katika mambo yala yala uika kwa vandu veenu, shaali iveekeri iuka kwa wayahudi. 15 Veveekeri ni wayahudi niivo valemuwaa Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni wayahudi ambavo veledudishirira dufumesha. Vemkundira Ruvaku na ni maadui kwa vandu voose. 16 Valedushiingia dutacheche na mataifa ili vakolie iokolewa. Matokeo yake ni kwamba veendelea sambi saavo.Mwisho ghadhabu yaasha dooka yaavo. 17 Sohoso, ndugu, duveekeri dwaatengana naanyo kwa mda mfuhi,kimwili, si katika moku. Dulefanya kwa uweso wedu kwa kua shauku iduve idholia fikiamu fyenu. 18 Kwa kfa duveekundi isha kwenu, nihani Paulo, kwa mara limu na mara ingi, dhakini ishetani liledushiingia. 19 Kwa kfa ijiamini ledu ni choiki kwa baadae, au furaha, au taji, kujivunia mbedhe sa Bwana wedu Yesu wakati wesha kwakwe?Je si nyooyo saidi shaa vo vengi? 20 Kwa kfa nyoonyo ni utukufu na furaha yedu.