Genesis 50

Genesis 50:1

Yusufu alifanya nini na mwili wa Israeli baada ya Israeli kufariki?

Yusufu alitia dawa mwili wa Israeli.

Genesis 50:4

Yusufu alitoa ombi gani kwa Farao kuhusu mazishi ya baba yake, na kwa nini alifanya ombi hili?

Yusufu aliomba aweze kwenda katika nchi ya Kaanani kumzika baba yake, kwa maana baba yake alimfanya aape.

Genesis 50:7

Nani aliondoka pamoja na Yusufu kumzika Israeli?

Maafisa wote wa Farao, washauri wa nyumba yake, maafisa waandamizi wa Misri, nyumba ya Yusufu, ndugu wa Yusufu, nyumba ya baba yake, na vibandawazi na wapanda farasi wote walikwenda na Yusufu.

Genesis 50:10

Wakaanani walisema nini walipomwona Yusufu pamoja na wale aliokuwa nao?

Wakaanani walisema ya kwamba hili lilikuwa tukio la huzuni sana kwa Wamisri.

Genesis 50:12

Yusufu na ndugu zake walikwenda wapi baadaya kumzika baba yao?

Yusufu na ndugu zake walirudi Misri.

Genesis 50:15

Ndugu wa Yusufu walikuwa na mashaka juu ya nini baada ya Israeli kufariki?

Ndugu zake Yusufu walikuwa na mashaka ya kwamba Yusufu angelipiza kisasi kwa maovu yote ndugu waliyofanya kwake.

Ndugu walimwomba Yusufu kufanya nini kuhusu makosa waliyoyafanya dhidi ya Yusufu?

Ndugu walimwomba Yusufu kuwasamehe kwa makosa waliyoyatenda dhidi ya Yusufu.

Genesis 50:18

Ndugu wa Yusufu walifanya nini walipokuja kwa Yusufu?

Walipokuja kwa Yusufu, ndugu zake Yusufu walianguka chini mbele zake.

Yusufu alisema ni wema gani ambao Mungu alifanya kupitia matendo maovu ya ndugu zake?

Yusufu alisema Mungu alifanya mema ya kuhifadhi maisha ya watu wengi.

Genesis 50:22

Yusufu aliishi muda gani?

Yusufu aliishi miaka mia moja na kumi.

Genesis 50:24

Yusufu alisema nini kinakaribia kutokea kwake?

Yusufu alisema ya kwamba alikaribia kufa.

Yusufu alisema ni ahadi gani ambayo Mungu angetimiza kwa uzao wa Israeli?

Yusufu alisema Mungu angekuja kwa watu na kuwaongoza katika nchi ambayo Mungu aliwaahidi kwa Abrahamu, Isaka na Yakobo.

Yusufu aliwafanya watu wa Israeli kuapa kuwa wangefanya?

Yusufu aliwafanya waape ya kuwa watabeba mifupa ya Yusufu kutoka Misri watakaondoka Misri.

Nini kilitokea kwa mwili wa Yusufu alipokufa?

Mwili wa Yusufu ulitiwa dawa na kuwekwa katika jeneza huko Misri.