1
Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.
2
Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.
3
Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi na mwisho wa siku 150 maji yakawa yamezama chini.
4
Safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.
5
Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
6
Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.
7
Akatuma kunguru na akaruka hadi maji yalipo kauka katika nchi.
8
Kisha akatuma njiwa kuona kama maji yamezama chini kutoka kwenye uso wa nchi,
9
lakini njiwa hakuona sehemu ya kutua unyayo wake, na akarudi kwake ndani ya safina, kwa kuwa maji yalikuwa bado yamefunika nchi yote. Akanyoosha mkono wake, akamchukua na kumuweka ndani ya safina pamoja naye.
10
Akasubiri siku saba zingine akatuma tena njiwa kutoka kwenye safina.
11
Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! Katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi.
12
Akasubiri siku saba zingine na akamtuma njiwa tena. Njiwa hakurudi kwake tena.