Sura 11
1
Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja.
2
Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale.
3
Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.
4
Wakasema, “Njooni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote.”
5
Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga.
6
Yahwe akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Karibuni, halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya.
7
Njooni, tushuke na tuvuruge lugha yao pale, ili kwamba wasielewane.”
8
Kwa hiyo Yahwe akawatawanya kutoka pale kwenda pande zote za uso wa nchi na wakaacha kujenga mji.
9
Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote.
10
Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa 100, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika.
11
Shemu akaishi miaka 500 baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike.
12
Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka 35 akamzaa Shela.
13
Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
14
Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Eberi.
15
Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
16
Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka 34, akamzaa Pelegi.
17
Eberi aliishi miaka 430 baada ya kumzaa Pelegi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
18
Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Reu.
19
Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumzaa Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
20
Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka 32, alimzaa Serugi.
21
Reu aliishi miaka 207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
22
Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Nahori.
23
Seregu aliishi miaka 200 baada ya kumzaa Nahori. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
24
Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka 29, akamzaa Tera.
25
Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
26
Baada ya Tera kuishi miaka 70, akamzaa Abram, Nahori, na Haran.
27
Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera aliwazaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu.
28
Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo.
29
Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska.
30
Sasa Sarai alikuwa tasa; hakuwa na mtoto.
31
Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale.
32
Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani.