Sura 1

1 Wia wedi, ambao ni wa Seemani. Mvyee mdodo akatamwiia na mpenzi ywakwe. 2 O, atinee kunibusu na mabusu ya muomo, wako kwa kua ukundiso wako ni wedi kuliko mvinyo. 3 Mavuta yako ya kwesisa yana manukato matana, zina dako denga malashi yeeyayo, ivyo wavyee wadodo wakukunda. 4 Nidoa kwako, na n'ndatiguuke. Mvyee akatamwiia mwenye Mfaume kanegaa mwe vyumba vyakwe. Mvyee akatamwiia na mpenzi ywako nina kinyemi, natamiwa kuhusu wewe, eka nishelehekee ukundiso wako; ni wedi kuliko mvinyo. Nihalisi kwa wavyee wekumwe kukunda. Mvyee akatamwiia na wavyee watuhu. 5 Mie akichuta mia ni mtana, nywie wana vivyee wa wagosi wa yelusalemu -mchuta inga hema za Kedili, muwatana inga mapazia ya Seemani. 6 Wesekwehewa kwa sibabu nkichuta kwa sibabu zua dinoka, wana wa mame nee wana mbifya uanga yangu, wanitenda mtunzi ya minda mizabibu, mia mnda wangu wa mizabibu nkizati kuutunduia. Mvyee akatamwiia na mpenzi ywakwe. 7 Nambia, we nikukundae, waisia hahi mifugo ywako? N'hahi ihumwiizaho mifugo yako musi? Kwa mbwai niwe inga muntu muangadika mweiyo mifugo ya wambuyazo? mpenzi yakwe akamtambaisa. 8 Kana nkumanya ekye mtana mweao wavyee, tongea majato ya mifugo ywangu, na uise wana mbuzi wako hehi na hema da waisi. 9 Nakuiganya mpenzi ywangu na falasi mtana ya kivyee mweao falasi wa magai ya falao. 10 Mafunda ywako ni matana na mahambo, singo yako na mikufu ya madini. 11 Nndanigosoee mahambo ya zahabu yekuhanganywayo na feza. Mvyee akatamwiia wenye. 12 Ukati mfaume akawa kagona mwe usazi wakwe, malashi yangu yakasawanya halufu. 13 Mpenzi ywangu ni kwangu inga kijauba cha malashi kigonacho nakio mwe matombo yangu. 14 Mpenzi wangu ni kwangu inga kabundu ka maua ya hena mwe minda ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi ywakwe atamwiia nae. 15 Kaua, we u mtana mpenzi ywangu; kaua, we u mtana, meso yako ni kana ya ngiwa Mvyee atamwiia na mpenzi ywake. 16 Kaua, we umtanda, mpenzi ywangu, jinsi mtanda. 17 Nguzo za nyumba yetu ni za matambi ya mielezi, na taa detu ni da matambi ya mibeloshi.