1 Basi Yakobo akamanya kua kuna nafaka uko Misri. Akawamba wanawe, "Kwa mbwai mwakauana? 2 Akagombeka, "Kaua, nkisikia kua kuna nafaka uko Misri. Seeani uko mkatiguie nkande ili tiishi waa tesekufa." 3 Ndugu kumi wa Yusufu wakaseea Misri kugua nkande. 4 Akini Benjamini, nduguye da Yusufu, Yakobo nkeekumtuma hamwe na nduguze, kwani kawa na wasiwasi kwa mazala yadaha kumpata. 5 Wana wa Israeli wakeza kugua mweao wekwezao kwanisaa nee iyaho mwe sii ya Kanaani. 6 Basi Yusufu nee ni mtawala juu ya juu yasii. Nee mwekuae akawatagia wantu wose wa sii. Nduguze da Yusufu wakeza na kumwenamia na vyeni vyao hata sii. 7 Yusufu akawaona nduguze na kuwamanya, akini kehitua na kutamwiia nao kwa ukai. Akawamba, "Muawa kuhi?" Wakagombeka, kuawa sii ya Kanaani teza kugua nkande." 8 Yusufu akawamanya nduguze, akini wowo nkawokummanya. 9 Yusufu akakumbuka sozi ekuiotayo kuhusu wowo. Akawamba, "Nywinywi mu wapelelezi. Mweza kuona mphaamo za sii zesazokuindwa." 10 Wakamwamba, "Chuu, bwana wangu. Wandima wako weza kugua nkande. 11 Swiswi wose ti wana wa tate yumwe. Ni wantu wa kwei. Wandima wako nkio wapelelezi.'' 12 Akawamba, "Chuu, mweza kukaua mphaamo za sii zesazokuindwa." 13 Wakagombeka, "Swiswi wandima wako timo ndugu kumi na waidi, wana wa tate yumwe mwe sii ya Kanaani. Kaua, mdodo kasigaa na tatietu, na mtuhu nkayumeso vituhu." 14 Yusufu akawamba, Nee nekumyambavyo; nywie mu wapelelezi. 15 N'ndamgeezwe kwa sia inu. Kana ekaavyo Farao, nkamnamhauke aha, mvuna yenu akesekweza aha. 16 mtumeni yumwe yenu akamweete mvuna yenu. N'ndamsigae geezani, hata mbui zenu ndiho zisibitishwe kua kuna ukwei ndani yenu." 17 Akawagea kifungoni kwa misi mitatu. 18 Mwe msi wa ntatu Yusufu akatamwiia nao. "Gosoani ivi nanywi nndamuishi, kwani namcha Mungu. 19 Kana nywinywi mu wantu wa kwei, yumwe yenu n'ndaazuiliwe aha hegeeza, akini nywinywi hiyani. Doani nafaka kwa ajii ya nyumba zenu. 20 mweeteni mvuna yenu kwangu ili kwamba mbui zenu zisibitishwe nanywi nkamnamfe." Wakagosoa ivyo. 21 Wakasemezana wowo kwa wowo, "Kwa kwei tina hatia juu ya ndugu yetu kwani tiiona tabu ya nafsi yakwe ekutisihiho naswi nkatokusikia. Kwa iyo tabu inu itiuwiiya." 22 Rubeni akawaandua, "Je ncheekumyambia, "Mwesekugosoa zambi juu ya kijana akini yakundigwa juu yenu." 23 Akini nkaokumanya ati Yusufu awamanya, kwani nee kuna mkalimani kati yao. 24 Akaawa ekuwaho uku aiya. Akauya kwao na kutamwiia nao. Akamdoa Simoni mweao na kumtaha mbele ya meso yao. 25 Akaawaaho yusufu akaagiiya wandima kumemeeza mifuko yao kwa nafaka; na kuvuza hea ya kia yumwe mwe guniadakwe, na kuwenka mahitaji kwa ntambo. Wakagosoewa ivyo. 26 Awa ndugu wakakweza nkande zao uanga ya mphunda wao na kuhauka hada. 27 Yumwe ekuchopoaho gunia dakwe ili kumuisa mphunda yao hada hantu wekuwaho, akaona hea yakwe. Kaua, nee ihemuomo wa gunia dakwe. 28 Akawamba nduguze, "Hea yangu ivuzwa. Kaua, i mwe gunia dangu. "Myoyo yao ikabadiliika wakahitukiana kia yumwe uku wakakama. Wakagombeka, "Ni mbwai iki ekutigoseacho Mungu?" 29 Wakaita kwa Yakobo, tatiyao mwe sii ya Kanaani na kumwambia yose yekuwapatayo. 30 Wakagombeka, "Yuda muntu, bwana wa sii, katamwiia naswi kwa ukai na kutifikiia kua ti wapelelezi mwe sii. 31 Tikamwambia, "Ti wantu wa kwei swiswi. Swiswi nkio wapelelezi. 32 Timo ndugu kumi na waidi, wana wa tate yumwe. Yumwe nkako meso vituhu na mvuna yetu ana tatietu mwe sii ya Kanaani." 33 Yuda muntu, zumbe ya sii, akatambia, "Kwa idi nondanimanye kua ni wantu wa kwei nywinywi. Mbadeni yumwe na yumwe mweao ndugu zenu, doani nkande kwa ajii ya saa mwe nyumba zenu, doani nkande kwa ajii yasaa mwe nyumba zenu na mhauke. 34 Mweteni mvuna yenu kwangu. Nee ndiho nimanye kua nywinywi nkio wapelelezi, akini ni wantu wa kwei. Nikaawaaho n'ndanimuekee ndugu yenu, na n'ndamgosoe biashaa mwe sii." 35 Ikawa wekuchopoaho magunia yao, na kaua, mfuko wa hea wa kia yumwe nee umwe gunia dakwe. Ukati wowo na tatiao wekuonaho mifuko yao ya hea, wakaogoha. 36 Yakobo tatiao akawamba, "Mnibanangia wana wao. Yusufu nkayumeso vituhu, Simoni kahauka, nanywi mmegaa Benjamini nae. Mbui izi zose ni mhitu kwangu." 37 Rubeni akawamba tatiakwe, kugombeka, "Wadaha kuwakoma wanangu waidi nikesekumvuza Benjamini kwako. Mwiike mwe mikono yangu, nami n'ndanimvuze vituhu kwako." 38 Yakobo akagombeka, "Mwanangu n'ndaasee hamwe na nywinywi. Kwani nduguye kaumbwa mzimu na yeye ukedu kasigaa. Ati mazala yondayampate mwe sia mwembokeayo, neendiho mziseeze afi zangu mwe kabui kwa huzuni."