Sura ya 30

1 Raheli ekuonaho nkamvyaia wana Yakobo, Raheli akamwonea wivu dadie. Akamwamba Yakobo, "Nenka wana, nkivyo nafa." 2 Hasira ya Yakobo kwa Raheli ikawa ni nkuu sana. Akamwamba, "Mimi ni badii ya Mungu, mwekukuzuia usekupata wana? 3 Akamwamba, kaua, kuna mjakazi wangu Bilha. Gona naye uwo utende me uvyazi wangu, nami nndanipate wanawe. 4 Ivyo akamwenka Bilha mjakazi kama mkaziwe, na Yakobo akagona naye. 5 Bilha akatoza mimba na kumvyaia Yakobo mwana. 6 Kisha Raheli akamba, "Mungu kaamua kwa faida yangu. Kayatetegeeza maombi yangu na kunenka mwana." Kwa ajii iyo yuda mwana akamwetanga Dani 7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akatoza mimba vituhu na kumvyaia Yakobo mwana ya kaidi. 8 Raheli akamba, "Kwa mashindano ya nguvu nenikashindana na dada nami nkimvota." Akamwetanga zina dakwe Naftali. 9 Lea ekuonaho nkavyaa vituhu, akamdoa Zilpa, mjakazi yakwe na kumwenka Yakobo yakwe na kumwenka Yakobo kama mkaziwe. 10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamvyaia Yakobo mwana. 11 Lea akamba, "Inu ni bahati ntana!" Kwa iyo akamwetanga zina dakwe Gadi. 12 Kisha Zilpa, mjakazi wa Lea, akamvyaia Yakobo mwana ya kaidi. 13 Lea akamba, "Nna furaha kwa maana mabinti nndawanetange furaha, kwa hiyo akamwetanga zina dakwe Asheri. 14 Mwe siku za mavuno ya ngano Rubeni akaita tanga na kuona ntunguja. Akamwetea mami yakwe, kisha Raheli akamwambia Lea, "Nenka baadhi ya izo ntunguja za mwanao.'' 15 Lea akamwamba, "Je ni mbui ndodo kwako, kwa kumdoa muumangu? Je na sasa wafaigwa n'kudoa ntunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, "Kisha undaugone nae ivyeo makio kwa kubadiishana na ntunguja za mwanao. 16 Guoni Yakobo akagotoka. Lea akenda kumhachiiza na kumwamba, ivyeo wagona na mimi, kwani nkikuajiri kwa ntunguja za mwanangu sa ivyo Yakobo akagona na Lea mwe kia kio. 17 Mungu akamsikia Lea, na akatoza mimba na kumvyaia Yakobo mwana ya shano. 18 Lea akamba, "Mungu kaniiha nekuavyo nikatigiwa, kwa sibabu nkimwenka muumangu mjakazi yangu." Akamwetanga zina dakwe Isakari. 19 Lea akatoza ifu vituhu na kuvya mwana ya shano kwa Yakobo. 20 Lea akamba, "Mungu kanenka zawadi ntana. Sasa muumangu andaniheshimu, kwa sibabu nkimvyaia wana sita." Akamwetanga zina dakwe Zabuloni. 21 Baadaye akapata kandee na kumwetanga zina dakwe Dina. 22 Mungu akamkumbuka Raheli na kundegeeza. Akapata ifu. 23 Akapata ifu na kuvyaa mwana, akamba, "Mungu kaniusia soni." 24 Akamwetanga zina dakwe Yusufu, uku asema, Yahwe kaniongezea mwana mtuhu." 25 Baada ya Raheli kumvyaa Yusufu, Yakobo akamwamba Labani, "Nieka niite, ili niite nyumbani kwetu na mwe si yangu. 26 Nenka wakazangu na wanangu nekukutumikiao kwa ajii yao, na unieke nihauke, kwani wamanye nekukutumikiavyo. 27 Labani akamwamba, "Kama undaunitegeeze, tuia, kwamba kwembokea wewe Yahwe kanibariki. 28 Kisha akamwamba, "Taja unitigiavyo nami nndanikuihe." 29 Yakobo akamwambia, "Wamanye nekukutumikiavyo, na jinsi ambavyo mfugo wako wekuavyo na mimi. 30 Ne ni wacheche kabla nkizati kweza na waongezeka kwa wingi. hohose nekukutumikiaho Mungu kanibariki. Je mpaka mwe ini nami ne andae kwa ajii ya nyumba yangu?" 31 Sa ivyo Labani akamwamba, "Je nikuihe mbwai? Yakobo akasema, usekunenka chochose. Na kama undaugosoe ivi kwa ajii yangu, nndaniwaise vituhu ngoto wako na kuwatunza. 32 Nieka ivyeo nemboke mwe dewa dako kwa kuusa kia ngoto mwenye mawakowako, na kia ngoto mzize, na kia mbuzi mwenye mawakowako. Awa wose ne ujira wangu. 33 Uadilifu wangu undaushuhudie kwa ajii yangu aho baadaye, ndiho weze ukaue ujira wangu. Kia ambaye nkana misitali na mzize mwe ngoto kama andaaonekane kwangu basi ni ya ubavi." 34 Labani akamba, "Nakubali. Na iwe kama usemavyo." 35 Kwa mtindo unu Labani akausa mabeberu yenye minjooza na mawako wako, na kia mwekua mweupe na mweusi kwa mbuzi akawakabidhi kwa wanawe. 36 Pia Labani akaahidi ntambo ya siku ntatu gatigati yakwe na Yakobo akabaki ne muisi wa ngoto wa Labani wekubakiao. 37 Yakobo akadoa matawi mawisi yekusengwayo ya mipopia, mlozi na mwaramoni muwisi akauusa maganda vyedi ida michiizi ingaayo ionekane, na akagosoa ivi mpaka ida sehemu ing'aayo ionekane mwe zia fito. 38 Kisha akazichovya mwe biika da mazi zia fito za minjooza wekwezaho kunywa mazi wada wanyama. Wakapata mimba wada wanyama. 39 Wakakweana mbele ya zia fito; wakavyaana wenye minjooza na mawakowako. 40 Yakobo akawaika nkandani na kundi da Labani. Kisha Yakobo akayatenga aya makundi yake mwenyewe pekee na hakuwaweka pamoja na wale wa Labani. 41 Wada wenye nguvu wekukweanaho akalaza zia fito ili kwamba watoze mimba. 42 Akini wada dhaifu wekwezaho nkekuvitenda ivyo, kwa hiyo ikawa wanyonge ni wa Labani na wenye nguvu ni wa Yakobo. 43 Mtu huyo akastawi sana. Akawa na kundi kubwa la kondoo, wajakazi na wajoli, ngamia na punda.